Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro limefanikiwa kumkamata Abubakary Mwichangwe (29), Dereva wa lori la mafuta lenye namba za usajili T.661BXW tela namba T.489 BHC ambaye alikuwa anatafutwa Kwa tuhuma za kuiba mafuta aina ya dizeli lita elfu 35 yenye thamani zaidi ya Tsh. milioni 77 kisha kulichoma moto gari hilo kwa lengo kupoteza ushahidi na yeye akatokomea kusikojulikana.
Kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro SACPnAlex Mkama amesema tukio hilo limetokea March 16,2025 katika Kijiji cha Msimba Wilaya kilosa Mkoani Morogoro barabara ya Morogoro - Iringa.
RPC Mkama amesema Mtuhumiwa aliiba mafuta kwa kula njama na Mameneja wa vituo vya mafuta kisha alipofika katika Kijiji cha Msimba aliliangusha gari korongoni na kujaribu kulichoma moto kabla ya Wasamaria wema kufika na kuzima na baada ya tukio Dereva alikimbia kusikojulika hadi baadaye Polisi walipomkamata ambapo Polisi haijasema imemkamata akiwa wapi kwasababu za kiupelelezi kwakuwa bado wengine aliokula nao njama kuchoma gari wanaendelea kusakwa.