Grace Mayemba, Ambaye Kwa Sasa Anafanya Kazi Ya
Kufundisha Lugha Ya Kingereza Huko Nchini Taiwani Amefanikiwa Kufikia Malengo
Yake Ya Muda Mrefu Ya Kusaidia Watoto Wa Kitanzania Wanoishi Kwenye Mazingira
Magumu Yanayowakwamisha Kupata Elimu Na Maarifa Katika Vijiji Mbalimbali Hapa
Nchini.
Grace Anasema Wazo La Kujenga Shule Na Chuo cha Ufundi Hapa Nchini
Lilitokana Na Changamoto Alizozibaini Kuwepo Kwenye Jamii Tangu Alipoanza
Masomo Yake Ya Shule Ya Msingi Katika Kijiji Cha Mkongotema Wilayani Madaba
Mkoani Ruvuma Mwaka1988 [Kwa Sasa Magingo Baada Ya Kijiji Mama Kugawanywa] Na
Kisha Kujiunga Na Sekondari Ya Ya Wilima Ambako Alihitimu Kidato Cha Nne Mwaka
1998 Na Baadae Akajiunga na Shule ya Sekondari Ya Kulipia Ya Mpechi Kwa Masomo
Ya Kitato Cha Tano Na Sita Mkoani Njombe mwaka 1999- 2000 Ambako Hakufanikiwa
Kuhitimu Kutokana Na Kukosa Ada Na Michango Mingine
Kutokana Na Ugumu Wa Maisha Kusoma Kwa Kumtegemea
Mama Yake Pekee Kwa Kuuza Pombe Ya Kienyeji Aina ya Ulanzi Grace Alienda Kuishi Kwa
ndugu Yake Jijini Dar es salamu Ambapo Badae Akajiunga Chuo na Cha Ualimu Vikindu Mkuranga
Mkoani Pwani Na Kisha Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania Tawi la Kinondoni Biafra Ambako Alisoma
Huku Akifanya Kazi Ya Ualimu Wa Shule za Msingi za serikali.
 |
Pombe aina ya ulanzi aliyouza bi Grace
Namamayakeili kupataada na michango |
Anasema Kwa Sehemu Kubwa Amejisomesha Yeye Mwenyewe
Kwa Kufanya Shughuli na kujituma Kwa Kufanya Kazi Mbalimbali za kujiingizia kipato tangu
akiwa Shule Ya Msingi Mpaka Chuo Kikuu Huku Akiwa amebeba Ndoto Kubwa Ya kujikwamua kimaisha yeye na
Jamii Ya Watanzania wenye hali kama yake.
‘’Nilisoma Kwa Shida Sana Baba Yangu Alifariki
Nikiwa Darasa La Tano Shule Ya Msingi Akiwa Ametuacha Watoto Saba Pamoja Na Mama Nilipojiunga Shule
Sekondari Wilima Kidato Cha Kwanza Hali IlikuaNgumu Sana Ikanilazimu Kufanya
Vibarua Vya Hapa Na Pale Ili Kupata Ada Na Mahitaji Mengine’’Alisimulia Grace Mayemba.
 |
Garace akifanya kibarua cha kusomba tofali huko kijiji cha mkongotema |
Baadae Grace Alijiunga Na Masomo YaMasters Nchini Taiwani katika chuo kikuu cha National Tsing Hua
Akisomea Lugha[ Masters of Linguistics ] Ambako Alihitimu mwaka 2023, pia alifanyia utafiti ya masomo
yake kwenye lugha ya a Kibena yenyemada ya ‘Tense Aspectand Modality in the Bena Language’. Na
Kisha Kupata Kazi ya kufundisha katika Moja Ya Shule Za Kiingereza za mfumo wa kimarekani Huko
Taiwani
 |
Picha Ni Grace Mayemba akiwana furaha Baada Ya Kuhitimu Masomo Ya Shahada Ya Uzamiri [Masters]
Huko nchini Taiwan aliyoisotea kwa miaka 4. |
KUHUSU NDOTO YA GRACE.
Katika Ndoto Yake Grace Anasema Aliweka nadhiri Kuwa aKifanikiwa Kwenye Maisha Yake Atahakikisha
Anajenga Shule Ambayo Itasaidia Mtoto Wa Kitanzania Kupata Elimu Katika Mazingira Rafiki Na Kwa
Gharama Nafuu Ndoto AmbayoImeanzaKutimia Ambapo KwaSasaAmeungana Na Rafiki Zakekutoka
Taiwani akiweno Winnie , Professor Perng, na Wataiwani Wengine Kujenga Shule Ya Msingi ya
Mchepuo WaKiingereza Na Chuo Cha Ufundi Stadi pamoja na hoteli Katika Kijiji Cha Magingo Wilayani
MadabaMkoaniRuvuma.

Shule Hiyo Pia Itasaidia Kupunguza Idadi Kubwa Ya Wanafunzi Katika Shule Za Msingi Za Serikali Huku
Chuo Kikitarajiwa Kupunguza Idadi Ya Vijana Wasio Na Ajira Baada Ya Kupata Ujuzi Wa Fani Mbalimbali
Hususani wale ambao hawataWezaKuendelea Na Masomo YaJuu.
Chuo Kitatoa Mafunzo Ya Hoteli , Kompyuta, Utalii, Umeme, Ufundi Bomba, ushonaji, Uandishi wa Habari,
Ualimu wa chekechea na Kutakua na Kozi Nyingine Zinazoweza Kuwapa Ujuzi Watanzania Kuweza
Kuajiriwa Na Kujiajiri kutokana na uhitaji.
KwaKuanza Grace Na Rafiki zake Wameanzisha Mradi WaKufanikisha Ndoto Hiyo Kubwa Unaoitwa
Alpha Tanzania Little dreamers’ big futures, Ambapo Katika Mradi Huo Kuna Wadau Mbalimbali Wanao
Jitolea Kufanikisha Ujenzi Wa Shule Hiyo Na Chuo cha ufundi Katika Kijiji Cha Magingo Wilayani Madaba
Mkoani Ruvuma
Hapo February 28 Mwaka 2025.
Wadau Kutoka Nchini Taiwani Na Tanzania Kutoka Mikoa Mbalimbali
Wamefanya Kikao Cha Kwanza Kwa Njia Ya Mtandao Kujadili Mambo Kadhaa Muhimu Ikiwemo Historia Ya
Wazo La Kujenga Shule [Ndoto Ya Grace] Kueleza Mradi Mzima Ulipo Fikia, Na Kuwasilisha Wazo La
Kujitolea kwa wadau hao Kikao Ambacho Kilikua Na Washiriki Nane ambao kwa pamoja walionyesha nia
ya kuhakikisha ndoto hiyo kubwa ya muda mrefu inafanikiwa kama kama yalivyo
matamanio ya dada Grace na rafiki zake.
 |
Wadau wakiwa katika mjadala kupitia mtandao |
Alpha Tanzania Kama Mradi Kwa Sasa Utakuwa Na Safu YaWafanyakazi WaKujitolea Na Viongozi Kutoka
Nchi Hizo Mbili Ambapo Grace Jenipher Mayemba Anakuwa Ni Mkurugenzi mkuu WaMradi Kutoka
Tanzania, Winnie ( 洪宜筠) Mkurugenzi WaMradiKwa Nchi yaTaiwan, BenLin (林元偉)-Mkuuwa
Idara ya Fedha Na Elimu, Kelly Mkuu wa Idara ya Tehama Na Angle kwok mkuu wa Idara ya ubunifu na
Matangazo upande wa Taiwani.
Mpaka Sasa Mradi Wa Alpha Tanzania Umefikia Hatua Nzuri Ambapo Umesha Pata Eneo La Kujenga
Shule Ya Msingi Ya Mchepuo Wa Kingereza Kijiji Cha Magingo eneo la kihoho Na Chuo Cha Ufundi eneo
la ukubwa wa ekari kumi (10).
Mradi Umepata ufadhili kutoka kwa Mr .Chen (陳炘陽) waKufikisha Umeme
Na Maji Kutoka Kijijini Mpaka Eneo La Ujenzi [Sight] Na Kujenga Msingi Wa Madarasa Sita Ya Shule Ya
Msingi.
‘’Tulipo Fika Kijiji cha Magingo Mimi Na Rafiki Zangu Kelly Na Winnie Tuliwaeleza Lengo La Kujenga Shule
Na Tukapewa Eneo La Kujenga Shule La Ukubwa Ekari 10 AmbaloTulilitembelea Na Kuona Linafaa
Kujenga Shule Ya Msingi Chuo Na Hoteli’’Grace
Kwa Mujibu Wa Grace Mayemba Jitihada Za Kufanikisha Ndoto Na Kupata Fedha Zinaendelea Kupitia
Wadau Kutoka Nchini Tanzania Na Taiwani Ambapo Anasema Anatamani Ndoto Hii Itimie Mpaka Ifikapo
Mwaka 2030 Kwa Kujenga Shule Ya Msingi Mchepuo Wa Kiingereza ,Chuo Cha Ufundi Stadi Na Hoteli
Katika Eneo Alilopewa Bure Na Serikali Ya Kijiji Cha Magingo Huko Mkoani Ruvuma Nchini Tanzania
Mradi Ambao Unakadiriwa Kugharimu Zaidi Ya Shilingi Bilion Mbili Za Kitanzania.
 |
PICHA Kulia ni eneo la kujenga shule ya msingi na chuo cha ufundi na kushoto ni badhi wajumbe wa serikali ya kijiji cha Magingo wilayani madaba mkoani Ruvuma. |