Ajinyonga siku moja baada ya kutoka kituo cha polisi

Adimin
0

 Athuman Idd (35), mkazi wa mtaa na Kata ya Ndembezi, Manispaa ya Shinyanga, amekutwa amejinyonga katika Kata ya Kolandoto siku moja baada ya kuachiwa kutoka Polisi.



Mwenyekiti wa mtaa wa Ndembezi, Mariam Mdoe, amesema kuwa tukio hilo limetokea siku moja baada ya marehemu kutoka polisi.

Amesema kuwa Jumamosi mwanamke mmoja alifika ofisini kwake akiomba barua ya dhamana kwa ajili ya mumewe aliyekuwa polisi.

Baada ya kuandika barua hiyo, mwanamke huyo alienda kumdhamini mumewe. Hata hivyo, siku iliyofuata, yaani Jumapili, alimtafuta kwa simu na kumjulisha kuwa mumewe amekutwa amejinyonga.

"Ilipofika Jumamosi, mwanamke mmoja alifika ofisini kwangu akiomba barua ya dhamana kwa ajili ya mumewe aliyekuwa polisi. Tulimwandikia, akaenda kumdhamini, lakini siku ya Jumapili alitupigia simu kutupa taarifa kuwa mumewe amefariki dunia baada ya kukutwa amejinyonga," amesema Mdoe.

Inaelezwa kuwa marehemu Athuman Idd, aliyekuwa na umri wa miaka 35, alikamatwa na polisi kwa kosa la kuendesha pikipiki akiwa amelewa na bila kuvaa kofia ngumu.

Jamii imeelezea masikitiko yake kuhusu tukio hilo na kuwaomba wananchi kuepuka kujichukulia sheria mkononi kwa kujitoa uhai, huku pia ikihimiza watu kuacha unywaji wa pombe kupita kiasi.

Marehemu ameacha mke na watoto watatu, hata hivyo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limesema bado halijapokea taarifa rasmi kuhusu tukio hilo
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Idawa Media Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top