Mwanaume mkazi wa kijiji cha Igelehedza, kata ya Ilembula, wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe, Erasto Raphaely Kabupa (50) amefariki dunia akiwa katika tukio la kushiriki tendo la ndoa na mwanamke mmoja, ambaye anadaiwa kuwa mke wa mtu.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe Mahamoud Banga amethibitisha kupokea taarifa za tukio hilo na kueleza kuwa lilitokea siku ya tarehe 8 juni 2025 kati ya saa moja jioni hadi saa mbili usiku, ambapo marehemu alikuwa na mwanamke huyo ambaye jina lake limehifadhiwa katika nyuma ya kulala wageni iliyopo Igelehedza ambapo wakati wakiendelea na tendo alizidiwa gafla na kukimbizwa kituo cha afya Ilembula na kukutwa ameshapoteza maisha.
Kamanda Banga amesema kutokana na aina ya tukio hilo jeshi la polisi haliwezi kumkamata mwanamke aliye kuwa pamoja na marehemu huyo,huku akitoa wito kwa wanandoa kuwa waaminifu na kuheshimu ndoa zao.
Diwani wa kata ya Ilembula Hezron Myale amesema kupitia taarifa ya familia ambayo imetolewa wakati wa mazishi ambayo yamefanyika leo imebainisha kuwa sababu ya kifo cha Eresto Kabupa ambaye pia ameacha mjane na watoto ni tatizo la moyo ambalo limekuwa likimsumbua kwa mda mrefu huku akiwataka wanandoa kuwa waaminifu kwenye ndoa zao ili kulinda uchumi na familia zao.
Baadhi ya wananchi mjini Makambako Pascal Shauri na Justini Mwanganya wamesema changamoto kubwa kwa sasa kwa wanandoa ni kukosa kuaminiana, maelewano na uvumilivu hali ambayo inapelekea kusalitiana na kuleta adha katika familia kwani visa vya mapenzi ndio sababu ya mauaji.
Erasto Kabupa ambaye alikuwa ni mwenye ulemavu wa miguu uliosababishwa na ajari enzi za uhai wake alikuwa akijishughulisha na shughuli za ufundi wa ushonaji viatu na baadaye usafirishaji abiria kwa kutumia bajaji kutoka ilembula kwenda halali.