Watu 28 wamefariki dunia na wengine tisa kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyotokea usiku wa Juni 7, 2025 majira ya saa mbili usiku, katika eneo la mteremko wa Mbalizi, mkoani Mbeya.
Ajali hiyo imetokea baada ya lori la mizigo kufeli breki na kugonga magari mawili yaliyokuwa mbele yake — daladala ya abiria na kirikuu (gari dogo la mizigo).
Kutokana na mgongano huo, daladala hiyo iliingia korongoni na baadaye lori hilo liliangukia juu yake, na kusababisha vifo vya abiria waliokuwemo ndani.
TAZAMA VIDEO HII YA AJALI
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa majeruhi tisa wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Teule ya Ifisi.