Klabu ya Singida Black Stars imemtangaza rasmi Miguel Gamondi kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Gamondi, ambaye aliwahi kuwa Kocha wa Klabu ya Yanga SC, anarudi Ligi Kuu ya Tanzania akiwa na kazi kubwa kuelekea msimu mpya wa mashindano wa 2025/2026.
Katika hatua hiyo hiyo, Kocha David Ouma na Kocha Moussa N’Daw wameteuliwa kuwa Makocha Wasaidizi wa Gamondi ambapo Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo imesema mabadiliko haya kwenye benchi la ufundi yamelenga kuimarisha kikosi na kuongeza ushindani msimu ujao