Amuua Mdogo wake wakichapana fimbo

Adimin
0

 Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa linamshikilia Mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza kutoka Shule ya Sekondari Mtenga, Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa, Samwel Kayoka (16) kwa tuhuma za mauaji ya mdogo wake Jackson Kayoka (14) kwa fimbo walipokuwa wakicheza mchezo wa kupigana kwa fimbo.


Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kwa njia ya Simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, SACP Shadrack Masija amesema tukio Hilo limetokea katika Kijiji cha Mtenga "A" wakati Watoto hao walipokuwa wakicheza kwa kupigana na fimbo, katika mchezo huo marehemu alipigwa na fimbo kichwani na kudondoka chini.

Amesema baada ya marehemu kuanguka chini na kupoteza fahamu alichukuliwa na kukimbizwa katika Zahanati ya Mtenga na wakati jitihada za kumpatia matibabu zikiendelea alipoteza maisha.

Kamanda Masija amedai Jeshi la Polisi kwa sasa linaendelea kumshikilia Mtoto huyo huku wakiendelea na uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo na kuwa baada ya hapo mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma hizo zinazomkabili.

Awali, Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Romwald Kapele alidai kuwa Watoto hao ni wa familia Moja na kuwa katika Mila ya Kabila la Wasukuma ni kawaida kwa kwa Watoto wa umri huo kucheza michezo ya namna hiyo ya kupigana kwa fimbo na kuwa hata baada ya tukio hilo kutokea mtoto anayetuhumiwa kuwa hakukimbia na badala yake alikuwa akishangaa tukio lenyewe.

Alidai baada ya taratibu mbalimbali za Kipolisi kufanyika ndugu walikabidhiwa mwili wa marehemu na taratibu za mazishi zimefanyika Julai 7, 2025.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top